بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمَٰنِ الرَّحِيمِ Kwa Jina La Mwenyezi Mungu, Mwingi Wa Rehema, Mwenye Kurehemu. |
87:1
سَبِّحِ اسْمَ رَبِّكَ الْأَعْلَى
*Litakase jina la Mola wako Mlezi aliye juu kabisa,
*Celebrate the Name of your Lord, the Most Exalted,
|
87:2
الَّذِي خَلَقَ فَسَوَّىٰ
*Aliye umba, na akaweka sawa,
*who created and proportioned,
|
87:3
وَالَّذِي قَدَّرَ فَهَدَىٰ
*Na ambaye amekadiria na akaongoa,
*who determined and guided,
|
87:4
وَالَّذِي أَخْرَجَ الْمَرْعَىٰ
*Na aliye otesha malisho,
*who brought forth the pasture,
|
87:5
فَجَعَلَهُ غُثَاءً أَحْوَىٰ
*Kisha akayafanya makavu, meusi.
*and then turned it into a black scum.
|
87:6
سَنُقْرِئُكَ فَلَا تَنْسَىٰ
*Tutakusomesha wala hutasahau,
*We shall have you recite, then you will not forget any of it
|
87:7
إِلَّا مَا شَاءَ اللَّهُ ۚ إِنَّهُ يَعْلَمُ الْجَهْرَ وَمَا يَخْفَىٰ
*Ila akipenda Mwenyezi Mungu. Hakika Yeye anayajua yaliyo dhaahiri na yaliyo fichikana.
*except what God may wish. Indeed, He knows what is open to view and hidden.
|
87:8
وَنُيَسِّرُكَ لِلْيُسْرَىٰ
*Na tutakusahilishia yawe mepesi.
*We shall smooth your way to [preach] the easiest [canon].
|
87:9
فَذَكِّرْ إِنْ نَفَعَتِ الذِّكْرَىٰ
*Basi kumbusha, kama kukumbusha kunafaa.
*So admonish, for admonition is indeed beneficial:
|
87:10
سَيَذَّكَّرُ مَنْ يَخْشَىٰ
*Atakumbuka mwenye kuogopa.
*he who fears will take admonition,
|
87:11
وَيَتَجَنَّبُهَا الْأَشْقَى
*Na atajitenga mbali nayo mpotovu,
*and the most wretched will shun it
|
87:12
الَّذِي يَصْلَى النَّارَ الْكُبْرَىٰ
*Ambaye atauingia Moto mkubwa.
*—he who will enter the Great Fire,
|
87:13
ثُمَّ لَا يَمُوتُ فِيهَا وَلَا يَحْيَىٰ
*Tena humo hatakufa wala hawi hai.
*then he will neither live in it, nor die.
|
87:14
قَدْ أَفْلَحَ مَنْ تَزَكَّىٰ
*Hakika amekwisha fanikiwa aliye jitakasa.
*Felicitous is he who purifies himself,
|
87:15
وَذَكَرَ اسْمَ رَبِّهِ فَصَلَّىٰ
*Na akakumbuka jina la Mola wake Mlezi, na akasali.
*celebrates the Name of his Lord, and prays.
|
87:16
بَلْ تُؤْثِرُونَ الْحَيَاةَ الدُّنْيَا
*Lakini nyinyi mnakhiari maisha ya dunia!
*Rather you prefer the life of this world,
|
87:17
وَالْآخِرَةُ خَيْرٌ وَأَبْقَىٰ
*Na Akhera ni bora na yenye kudumu zaidi.
*while the Hereafter is better and more lasting.
|
87:18
إِنَّ هَٰذَا لَفِي الصُّحُفِ الْأُولَىٰ
*Hakika haya yamo katika Vitabu vya mwanzo,
*This is indeed in the former scriptures,
|
87:19
صُحُفِ إِبْرَاهِيمَ وَمُوسَىٰ
*Vitabu vya Ibrahimu na Musa.
*the scriptures of Abraham and Moses.
|