Sura 76 - Al-Insaan

بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمَٰنِ الرَّحِيمِ
Kwa Jina La Mwenyezi Mungu, Mwingi Wa Rehema, Mwenye Kurehemu.

76:1
هَلْ أَتَىٰ عَلَى الْإِنْسَانِ حِينٌ مِنَ الدَّهْرِ لَمْ يَكُنْ شَيْئًا مَذْكُورًا
*Hakika kilimpitia binaadamu kipindi katika zama ambacho kwamba hakuwa kitu kinacho tajwa.
*Has there been a period of time for man when he was not anything worthy of mention?
76:2
إِنَّا خَلَقْنَا الْإِنْسَانَ مِنْ نُطْفَةٍ أَمْشَاجٍ نَبْتَلِيهِ فَجَعَلْنَاهُ سَمِيعًا بَصِيرًا
*Hakika Sisi tumemuumba mtu kutokana na mbegu ya uhai iliyo changanyika, tumfanyie mtihani. Kwa hivyo tukamfanya mwenye kusikia, mwenye kuona.
*Indeed We created man from the drop of a mixed fluid so that We may put him to test, so We endowed with hearing and sight.
76:3
إِنَّا هَدَيْنَاهُ السَّبِيلَ إِمَّا شَاكِرًا وَإِمَّا كَفُورًا
*Hakika Sisi tumembainishia Njia. Ama ni mwenye kushukuru, au mwenye kukufuru.
*Indeed We have guided him to the way, be he grateful or ungrateful.
76:4
إِنَّا أَعْتَدْنَا لِلْكَافِرِينَ سَلَاسِلَ وَأَغْلَالًا وَسَعِيرًا
*Hakika Sisi tumewaandalia makafiri minyororo na pingu na Moto mkali.
*Indeed for the faithless We have prepared chains, iron collars, and a blaze.
76:5
إِنَّ الْأَبْرَارَ يَشْرَبُونَ مِنْ كَأْسٍ كَانَ مِزَاجُهَا كَافُورًا
*Hakika watu wema watakunywa katika vinywaji vilivyo changanyika na kafuri,
*Indeed the pious will drink from a cup seasoned with Kafur,
76:6
عَيْنًا يَشْرَبُ بِهَا عِبَادُ اللَّهِ يُفَجِّرُونَهَا تَفْجِيرًا
*Ni chemchem watakao inywa waja wa Mwenyezi Mungu, wakiifanya imiminike kwa wingi.
*a spring where Allah’s servants will drink, making it gush forth as they please.
76:7
يُوفُونَ بِالنَّذْرِ وَيَخَافُونَ يَوْمًا كَانَ شَرُّهُ مُسْتَطِيرًا
*Wanatimiza ahadi, na wanaiogopa siku ambayo shari yake inaenea sana,
*They fulfill their vows and fear a day whose ill will be widespread.
76:8
وَيُطْعِمُونَ الطَّعَامَ عَلَىٰ حُبِّهِ مِسْكِينًا وَيَتِيمًا وَأَسِيرًا
*Na huwalisha chakula, juu ya kukipenda kwake, masikini, na yatima, na wafungwa.
*For the love of Him, they feed the needy, the orphan and the prisoner,
76:9
إِنَّمَا نُطْعِمُكُمْ لِوَجْهِ اللَّهِ لَا نُرِيدُ مِنْكُمْ جَزَاءً وَلَا شُكُورًا
*Hakika sisi tunakulisheni kwa wajihi wa Mwenyezi Mungu. Hatutaki kwenu malipo wala shukrani.
*[saying,] ‘We feed you only for the sake of Allah. We desire no reward from you, nor thanks.
76:10
إِنَّا نَخَافُ مِنْ رَبِّنَا يَوْمًا عَبُوسًا قَمْطَرِيرًا
*Hakika sisi tunaiogopa kwa Mola wetu Mlezi hiyo siku yenye shida na taabu.
*Indeed we fear a frowning and fateful day from our Lord.’
76:11
فَوَقَاهُمُ اللَّهُ شَرَّ ذَٰلِكَ الْيَوْمِ وَلَقَّاهُمْ نَضْرَةً وَسُرُورًا
*Basi Mwenyezi Mungu atawalinda na shari ya siku hiyo, na atawakutanisha na raha na furaha.
*So Allah saved them from that day’s ills and graced them with freshness [on this faces] and joy [in their hearts].
76:12
وَجَزَاهُمْ بِمَا صَبَرُوا جَنَّةً وَحَرِيرًا
*Na atawajazi Bustani za Peponi na maguo ya hariri kwa vile walivyo subiri.
*He rewarded them for their patience with a garden and [garments of] silk,
76:13
مُتَّكِئِينَ فِيهَا عَلَى الْأَرَائِكِ ۖ لَا يَرَوْنَ فِيهَا شَمْسًا وَلَا زَمْهَرِيرًا
*Humo wataegemea juu ya viti vya enzi, hawataona humo jua kali wala baridi kali.
*reclining therein on couches, without facing any [scorching] sun, or [biting] cold.
76:14
وَدَانِيَةً عَلَيْهِمْ ظِلَالُهَا وَذُلِّلَتْ قُطُوفُهَا تَذْلِيلًا
*Na vivuli vyake vitakuwa karibu yao, na mashada ya matunda yataning´inia mpaka chini.
*Its shades will be close over them and its clusters [of fruits] will be hanging low.
76:15
وَيُطَافُ عَلَيْهِمْ بِآنِيَةٍ مِنْ فِضَّةٍ وَأَكْوَابٍ كَانَتْ قَوَارِيرَا
*Na watapitishiwa vyombo vya fedha na vikombe vya vigae,
*They will be served around with vessels of silver and goblets of crystal
76:16
قَوَارِيرَ مِنْ فِضَّةٍ قَدَّرُوهَا تَقْدِيرًا
*Vya fedha safi kama kiyoo, wamevipima kwa vipimo.
*—crystal of silver— [from] which they will dispense in a precise measure.
76:17
وَيُسْقَوْنَ فِيهَا كَأْسًا كَانَ مِزَاجُهَا زَنْجَبِيلًا
*Na humo watanyweshwa kinywaji kilicho changanyika na tangawizi.
*They will be served therein with a cup of a drink seasoned with Zanjabeel,
76:18
عَيْنًا فِيهَا تُسَمَّىٰ سَلْسَبِيلًا
*Hiyo ni chemchem iliyo humo inaitwa Salsabil.
*from a spring in it named Salsabeel.
76:19
وَيَطُوفُ عَلَيْهِمْ وِلْدَانٌ مُخَلَّدُونَ إِذَا رَأَيْتَهُمْ حَسِبْتَهُمْ لُؤْلُؤًا مَنْثُورًا
*Na watawazungukia kuwatumikia wavulana wasio pevuka, ukiwaona utawafikiri ni lulu zilizo tawanywa.
*They will be waited upon by immortal youths, whom, were you to see them, you will suppose them to be scattered pearls.
76:20
وَإِذَا رَأَيْتَ ثَمَّ رَأَيْتَ نَعِيمًا وَمُلْكًا كَبِيرًا
*Na utakapo yaona, utakuwa umeona neema na ufalme mkubwa.
*As you look on, you will see there bliss and a great kingdom.
76:21
عَالِيَهُمْ ثِيَابُ سُنْدُسٍ خُضْرٌ وَإِسْتَبْرَقٌ ۖ وَحُلُّوا أَسَاوِرَ مِنْ فِضَّةٍ وَسَقَاهُمْ رَبُّهُمْ شَرَابًا طَهُورًا
*Juu yao zipo nguo za hariri laini za kijani kibichi, na hariri nzito ya at´ilasi. Na watavikwa vikuku vya fedha, na Mola wao Mlezi atawanywesha kinywaji safi kabisa.
*Upon them will be cloaks of green silk and brocade and they will be adorned with bracelets of silver. Their Lord will give them to drink a pure drink.
76:22
إِنَّ هَٰذَا كَانَ لَكُمْ جَزَاءً وَكَانَ سَعْيُكُمْ مَشْكُورًا
*Hakika haya ni malipo yenu; na juhudi zenu zimekubaliwa.
*[They will be told]: ‘This is your reward, and your efforts have been well-appreciated.’
76:23
إِنَّا نَحْنُ نَزَّلْنَا عَلَيْكَ الْقُرْآنَ تَنْزِيلًا
*Hakika Sisi tumekuteremshia Qur´ani kidogo kidogo.
*Indeed We have sent down to you the Quran in a gradual descent.
76:24
فَاصْبِرْ لِحُكْمِ رَبِّكَ وَلَا تُطِعْ مِنْهُمْ آثِمًا أَوْ كَفُورًا
*Basi ngojea hukumu ya Mola wako Mlezi wala usimt´ii miongoni mwao mwenye dhambi au mwenye kufuru.
*So submit patiently to the judgement of your Lord and do not obey any sinner or ingrate from among them,
76:25
وَاذْكُرِ اسْمَ رَبِّكَ بُكْرَةً وَأَصِيلًا
*Na likumbuke jina la Mola wako Mlezi asubuhi na jioni;
*and celebrate the Name of your Lord morning and evening,
76:26
وَمِنَ اللَّيْلِ فَاسْجُدْ لَهُ وَسَبِّحْهُ لَيْلًا طَوِيلًا
*Na usiku msujudie Yeye, na umtakase usiku, wakati mrefu.
*and worship Him for a watch of the night and glorify Him the night long.
76:27
إِنَّ هَٰؤُلَاءِ يُحِبُّونَ الْعَاجِلَةَ وَيَذَرُونَ وَرَاءَهُمْ يَوْمًا ثَقِيلًا
*Kwa hakika watu hawa wanapenda maisha ya kidunia, na wanaiacha nyuma yao siku nzito.
*Indeed they love this transitory life, and disregard a heavy day that is ahead of them.
76:28
نَحْنُ خَلَقْنَاهُمْ وَشَدَدْنَا أَسْرَهُمْ ۖ وَإِذَا شِئْنَا بَدَّلْنَا أَمْثَالَهُمْ تَبْدِيلًا
*Sisi tumewaumba, na tukavitia nguvu viungo vyao. Na tukitaka tutawabadilisha mfano wao wawe badala yao.
*We created them and strengthened their joints, and We will replace them with others like them whenever We like.
76:29
إِنَّ هَٰذِهِ تَذْكِرَةٌ ۖ فَمَنْ شَاءَ اتَّخَذَ إِلَىٰ رَبِّهِ سَبِيلًا
*Hakika haya ni mawaidha; basi anaye taka atashika Njia ya kwenda kwa Mola wake Mlezi.
*This is indeed a reminder. So let anyone who wishes take the way toward his Lord.
76:30
وَمَا تَشَاءُونَ إِلَّا أَنْ يَشَاءَ اللَّهُ ۚ إِنَّ اللَّهَ كَانَ عَلِيمًا حَكِيمًا
*Wala hamwezi kutaka ila atakapo Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye ilimu, Mwenye hikima.
*But you will not wish unless it is willed by Allah. Indeed Allah is all-knowing, all-wise.
76:31
يُدْخِلُ مَنْ يَشَاءُ فِي رَحْمَتِهِ ۚ وَالظَّالِمِينَ أَعَدَّ لَهُمْ عَذَابًا أَلِيمًا
*Humuingiza amtakaye katika rehema yake. Na wenye kudhulumu amewawekea adhabu iliyo chungu.
*He admits whomever He wishes into His mercy, and He has prepared a painful punishment for the wrongdoers.